Tanzania yafungua kituo cha uhamiaji kilichojengwa na ufadhili kutoka Japan

21 Februari 2012

Taifa la Tanzania linatarajiwa kufungua makao mapya ya uhamiaji na polisi kwenye eneo la Kilwa Masoko na Kilwamba yaliyojengwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM ikiwa ni sehemu ya mradi wa uhamiaji uliofadhiliwa na serikali ya Japan. Mradi huo ulianzishwa ili kuwasaidi wahamiaji waliokwama hasa kutoka kwa pembe ya Afrika wanaopitia Tanzania wakiwa na lengo la kutafuta ajira nchini Afrika Kusini.

Utafiti uliofanywa mwaka 2009 na IOM ulionyesha kwamba kati ya vijana 17,000 na 20,000 kutoka Somalia na Ethiopia wanapitishwa nchini Tanzania wakielekea nchini Afrika Kusini kila mwaka. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM na alizungumza na Radio ya Umoja kuhusu ujenzi wa makao haya.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter