Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa dunia kujadili hatma ya Somalia mjini London

Viongozi wa dunia kujadili hatma ya Somalia mjini London

 

Viongozi kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanatarajiwa kukutana mjini London juma hili ili kujadili hatma ya taifa la Somalia ambalo kwa muda wa zaidi ya miaka 20 iliyopita limekumbwa na mapigano na kupelekea mamilioni ya watu kuhama makwao suala ambalo pia limechangiwa na ukame pamoja na njaa. 

Taifa la Kenya ambalo linapakana na Somalia ndilo makao kwa zaidi wa wakimbizi 500,000 kutoka Somalia wakati asilimia kubwa wanaishi kwenye kambi ya Dadaab. Kambi hiyo iliyo na uwezo wa kuwapa makoa wakimbizi 90,000 kwa sasa ni makoa kwa wakimbizi 463,000. Andrej Mahecic kutoka UNHCR anasema kuwa ukosefu wa usalama , utekaji nyara wa watoa misaada , misongangamano na mafuriko hufanya maisha kwenye kambi hiyo kuwa magumu.