Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saudi Arabia yatoa misaada ya kufadhili huduma kwa wakimbizi wa kipalestina

Saudi Arabia yatoa misaada ya kufadhili huduma kwa wakimbizi wa kipalestina

Taifa la Saudi Arabia kupitia kwa mfuko wa maendeleo wa taifa hilo umetoa msaada wa dola milioni kumi kufadhili mipango ya shirika la kuwahudumia wakimbizi wa kipalestina kwenye ukanda wa Gaza na ukingo wa Magharibi. Makubaliano hayo yalitiwa sahihi hii leo mjini Riyadh na fedha hizo zitatumika katika kununua vifaa vinavyohitajika kwenye elimu kama vile tarakilishi na vitabu.

Fedha hizo pia zitafadhili ukarabati wa vituo vya afya na kununua madawa na vyombo vingine vinavyotumiwa kwenye matibabu. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)