Ulimwengu usio na zana za nyuklia ndio salama:Ban

17 Februari 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ulimwegu utakuwa salama zaidi bila ya silaha za kinyuklia. Akiongea mjini Vienna Ban amesema kuwa mikataba ya kumaliza zana za kinyuklia ni muhimu katika kuleta amani duniani.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ban alikuwa akuhutubia mkutano wa kusherekea miaka 15 tangu kutolewa marufuku ya majaribio ya silaha za kinyuklia. Zaidi ya nchi 180 zimetia sahihi mkataba huo unaopiga marufuku silaha za kinyuklia kila eneo la dunia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud