Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yawalazimu wakimbizi kurudi tena mjini Mogadishu

Mapigano yawalazimu wakimbizi kurudi tena mjini Mogadishu

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema kuwa maelefu ya wakimbizi wa ndani waliohama makwao nchini Somalia kwa sasa wanazidi kuukimbia mzozo katika eneo la Afgooye lililo Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu Mogadishu. Eneo la Afgooye lililo na barabara yenye urefu wa kilomita 40 iliyo na kambi ni makao kwa karibu watu 410,000 wakimbizi wa ndani.

UNHCR inasema kuwa zaidi ya wakimbizi wa ndani 5200 wamekimbia eneo hilo kwa muda wa siku tatu zilizopita kufuatia ghasia zilizoshuhudiwa tangu siku ya Jumanne. Melissa Fleming kutoka UNHCR anasema kuwa wanaokimbia ghasia wanarejea tena mji wa Mogadishi mji walioukimbia awali.

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)