Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Finland zaongoza takwimu za UNCTAD za taarifa na teknolojia ya mawasiliano

Finland zaongoza takwimu za UNCTAD za taarifa na teknolojia ya mawasiliano

Finland inaongoza duniani kwa mchango wake wa kichumi utokanao na uzalishaji wa bidhaa na huduma zinazohusiana na taarifa na teknolojia ya mawasiliano ICT, kwa mujibu wa takwimu za karibuni zilizotolewa na tume ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD.

Takwimu hizo zilizotolewa Jumatano kwenye mtandao zinaonyesha kwamba teknolojia ya mawasiliano nchini Finland inatoa ajira kwa karibu 1/10 ya ajira zote zisizo za sekta ya kilimo nchini humo. Hata hivyo takwimu hizo zinasema sekta ya ICT ikiwemo upatikanaji wa takwimu bado ni duni katika nchi nyingi zinazoendelea.

UNCTAD inasema hadi sasa ina taarifa za nchi 57 tuu, na imeongeza kuwa ukosefu wa takwimu za kutosha unaweza kuonekana kama kikwazo kingine katika maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Na imesisitiza kuwa hakuna nchi hata moja kati ya zile masikini kabisa ambayo inatoa takwimu za ukubwa wa sekta zake za ICT.