Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sera za Israel kuzuia haki ya kuwa na nyumba:Rolnik

Sera za Israel kuzuia haki ya kuwa na nyumba:Rolnik

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na nyumba Raquel Rolnik ameonya kwamba hatua ya hivi majuzi ya ubinafsishaji wa mali ya serikali nchini Israel kumesababisha kuwepo kwa sera zinazowazuia wenye kipato cha chini kupata makao suala linalochangia kukiukwa kwa haki zao.

Akikamilisha ziara ya wiki mbili nchini Israel na kwenye ya kipalestina yanayokaliwa na Israel Rolnik amesema kwa sera za nyumba nchini Isreal zinahitaji kufanyiwa mabadiliko ya haraka. Rolnik ameongeza kuwa wapalestina wanaoishi nchini Isreal pamoja na wanaoishi kwenye ardi inayokaliwa na Israel kwa sasa haki zao za kuwa na nyumba ziko kwenye hatari. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)