Hiki ni kipindi muhimu sana kwa Israel na eneo zima la Mashariki ya kati:Ban

1 Februari 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amefanya mazungumzo na Rais wa Israel Shimon Peres mjini Jerusarem Jumatano. Ban na Peres wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo changamoto za hali ya Mashariki ya Kati. Ban amesema ushirikiano wa Israel katika kuleta tangamano kwenye eneo la Mashariki ya Kati ni muhimu sana, kwani Rais Peres amekuwa msitari wa mbele kuchagiza mchakato wa amani na pia muungaji mkono amani Mashariki ya Kati. Ban ambaye pia amejadili njia gani zitumike na Umoja wa Mataifa na jumuiya aa Kimataifa ambazo zinaweza kusaidia mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati. Kwani amesema huu ni wakati muhimu sana kwa Israel na eneo zima.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ameongeza kuwa bado anshawishika kwamba Israel inaweza kutoa mchango mzuri katika mabadiliko na kuimarisha uhusiano na jirani zake, ikiwa ni pamoja na kujihusiha kwenye mchakato wa amani na Palestina.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter