Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi kubwa ya Waafrika wanakufa wakivuka bahari ya Mediteranian:UNHCR

Idadi kubwa ya Waafrika wanakufa wakivuka bahari ya Mediteranian:UNHCR

Zaidi ya wahamiaji wa Kiafrika 1500 wamezama au kutoweka wakijaribu kuvuka bahari ya Mediteranian kuingia Ulaya mwaka 2011 limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Hii ni idadi kubwa kabisa ya vifo katika eneo hilo tangu mwaka 2006. UNHCR inasema mgogoro nchini Libya na Tunisia umesukuma idadi kubwa ya wahamiaji wapatao 58,000 kuwasili Ulaya kupitia bahari ya Mediteranian.

Sybella Wilkes kutoka UNHCR anasema wale walionusurika katika safari hizo wameelezea mswaibu yaliyowakuta ikiwa ni pamoja na kulazimishwa na walinzi wenye silaha kuchuka boti hasa wakati wa mgogoro wa Libya Aprili na Mai mwaka jana.

(SAUTI YA SYBELLA WILKES)

Tangu kuanza mwaka 2012 boti tatu zilizosheheni wahamiaji zimearifiwa kujaribu kuvuka toka Libya kuingia Ulaya. UNHCR inasema boti moja iliyokuwa na wahamiaji wa Kisomali 55 ilizama kabla ya kufika ilikokuwa inakwenda, maiti 15 ikiwemo ya mtoto mdogo wa kike zimepatikana.