Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pamoja na mkwamo wa kiuchumi mwaka uliopita lakini kiwango cha uwekezaji kiliongezeka-UM

Pamoja na mkwamo wa kiuchumi mwaka uliopita lakini kiwango cha uwekezaji kiliongezeka-UM

Kulingana na takwimu mpya zilizotolewa na Umoja wa Mataifa, hali ya uvuatiaji wawekezaji katika kipindi cha mwaka 2011 kilikuwa cha kuridhisha kikikuwa kwa kiwango cha asilimia 17 pamoja na kushuhudiwa hali ya mkwamo wa kiuchumi.

Ripoti hiyo inasema kuwa kiwango hicho cha kuridhisha kinatazamiwa kushuhudiwa pia katika kipindi cha mwaka huu lakini imeonya juu ya kile ilichokiita hali mbaya inayoweza kuindama sekta ya uchumi.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, kiwango cha uwekezaji kilikuwa kwa kiwango cha asilimia 17 huku nchi zilizoko katika eneo la Latin Amerika ndizo zikichukua fursa nzuri zaidi kwa kuitia wawekezaji wengi zaidi.

Nchi zinazoibukia kiuchumi ambazo miaka mitatu ya nyuma ziliporomoka kwa kuvutia idadi ndogo ya wawekezaji, safari hii zimeimarika na zinatarajiwa pia kufanya vizuri ndani ya mwaka huu.