ICC yaweka tarehe ya kutangazwa kwa hatma ya washukiwa sita raia wa Kenya

20 Januari 2012

Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ya ICC imetangaza kuwa itatoa uamuzi wake kuhusu washukiwa sita raia wa Kenya mnamo Januari 23 mwaka huu wakiwemo wagombea wawili wa urais Uhuru Kenyatta na William Ruto ikiwa wana kesi za kujibu kwenye mahakama hiyo.

Kutajwa kwa kesi za washukiwa hao kulifanyika mara mbili kati ya tarehe mosi hadi 8 mwezi Septemba mwaka 2011 na tarehe 21 hadi tano mwezi Oktoba mwaka uliopita. Uamuzi huo utatolewa kabla ya majaji wa mahakama ya ICC kutangaza matokeo ya uamuzi wao. Hakuna mshukiwa yeyote  atakuwa mahakamani wakati wa kutolewa kwa uamuzi huo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud