Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM ataka utawala wa Korea Kaskazini kughulikia masuala ya haki za binadamu

Mtaalamu wa UM ataka utawala wa Korea Kaskazini kughulikia masuala ya haki za binadamu

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki za binadamu nchini Korea Kaskazini ameutaka utawala mpya nchini Korea Kaskazini kushughulikia masuala ya haki za binadamu na kutatua matatizo ya muda mrefu yakiwemo kutekwa nyara kwa raia wa Japan na raia wa nchi zingine.

Akimaliza ziara rasmi nchini Japan Marzuki Darusman amesema ushirikiano kutoka Korea Kaskazini na jamii ya kimataifa utakaribishwa kama ilivyofanyika kwa taifa la Myanmar ambapo mabadiliko yake yamekaribishwa. George Njogopa anaripoti.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)