Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watu waliohama makwao kwenye jimbo Jonglei yaongezeka

Idadi ya watu waliohama makwao kwenye jimbo Jonglei yaongezeka

Mratibu wa masuala ya haki za binadamu nchini Sudan Kusini Bi Lise Grande amedhibitisha kuwa zaidi ya watu 120,000 walioathiriwa na mapigano ya hivi majuzi kwenye jimbo la Jonglei wanahitaji misaada ya dharura. Mapigano kati ya jamii ya Lou Nuer na Murle yalisambaa mwezi Disemba na kusababisha maelfu ya watu kuhama makwao , vifo na uharibifu wa mali.

Shambulizi la hivi majuzi lilifanyika Januari 16 ambapo watu 80 waliripotiwa kuuawa na nyumba 300 kuchomwa. Mashirika ya kibinadamu yanajaribu kukarabati vituo vuya maji na kutoa misaada ya chakula, bidhaa za nyumbani, lishe na huduma za afya.