Mapigano mpya yasababisha kuhama kwa watu 100,000 nchini DRC

Mapigano mpya yasababisha kuhama kwa watu 100,000 nchini DRC

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa zaidi ya watu 100,000 wamelazimishwa kuhama makwao Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kufuatia kutokea kwa mapigano mapya kati ya vikosi vya serikali na makundi ya waasi. Takriban watu 35,000 wamelazimika kuhama makwao kutoka maeneo ya walikale na Masisi mkoani Kivu Kaskazini.

UNHCR inasema kuwa Takriban watu 22 wameuawa na idadi ya wanawake isiyojulikana kubakwa wakati wa mapigano hayo. Adrian Adwards kutoka UNHCR anasema kuwa ukosefu wa usalama kwenye maeneo yaliyoathirika kumezuia kusafirishwa kwa misaada ya kibinadamu kwa waliohama makwao.

(ADRIAN EDWARDS)