Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Johnson apongeza mabadiliko ya kisiasa nchini Sudan Kusini

Johnson apongeza mabadiliko ya kisiasa nchini Sudan Kusini

Mjumbe maalum wa katibu mkuu nchini Sudan Kusini Hilde Johnson ametaka kumalizika kwa mizozo kwenye taifa hilo jipya na kutoa wito kwa serikali kuwafikisha mbele ya sheria wahusika na pia kupeleka vikosi zaidi kwenye maeneo ya mizozo ili kuzuia umwagaji wa damu.

Amesema kuwa kuendelea kuwepo hali mbaya ya usalama kwenye jimbo la Jonglei ni mtihani kwa wote akiongeza kuwa jitihada zinazostahili kufanywa ni kumaliza mizozo iliyopo ambayo inahatarisha maisha ya maelfu ya watu na usalama wa eneo lote.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Bi Johnson amelaani matamshi ya uchochezi yanayotolewa na watu binafsi na pia makundi ya watu.

Mapigano mabaya kati ya jamii ya Lou Nuer na murle kwa majuma machache yaliyopita yamewalazimu maelfu ya watu kuahama makwao na kupekea mashirika ya UM kuandaa oparesheni za kibinadamu kuwasaidia walioathiriwa.