Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la kimataifa la elimu la ainisha vigezo vya mafanikio

Kongamano la kimataifa la elimu la ainisha vigezo vya mafanikio

Kongamano la kimataifa la elimu limeanza Jumatatu Januari 9 mjini London na litaendelea hadi Januari 11 mwaka huu amesema mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO.

Bi Bokova anatarajiwa kutoa hotuba maalumu Jumanne na kuwasilisha mkakati wa mafanikio ya elimu kwa waalimu.

Katika hotuba yake Bi Bokova atatoa msisitizo wa haja ya kuwa na suluhu ya “kwenda sambamba na mahitaji” akifafanua kwamba kupiga hatua ni zaidi ya suala la fedha kinachohitajika ni kuweza kukidhi mahitaji, na kuwa na ujuzi unaostahili, na lazima watu wawe wabunifu ili kuweza kufanikiwa katika elimu.

Takriban mawaziri wa elimu 60 wanahudhuria kongamano hilo ambapo pia litatathimini wapia ambako hata zimepigwa haraka katika upande wa elimu na kuonyesha umuhimu wa sera za elimu na mikakati ambayo inaleta mafanikio.