Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini inahitaji mshikamano kushughulikia changamoto za kibinadamu:Guterres

Sudan Kusini inahitaji mshikamano kushughulikia changamoto za kibinadamu:Guterres

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Antonio Guterres amesema shirika hilo linajihusisha moja kwa moja kuwasaidia wakimbizi na watu wengine waliotawanywa na machafuko Sudan Kusini.

Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa Guterres ambaye yuko ziarani Sudan Kusini amesema UNHCR na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa yanafanya kila liwezekenalo ili kuwalinda raia nchini humo. Ameongeza hata hivyo mshikamano unahitajika ili taifa hilo jipya liweze kushughulikia changamoto za kibinadamu. Bwana Guterres pia amepongeza mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini UNMIS kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuzuia kuendelea kwa machafuko.

(SAUTI YA ANTONIO GUTERRES)