Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchezo wa mtandao wa kupiga vita njaa wapata washirika milioni moja

Mchezo wa mtandao wa kupiga vita njaa wapata washirika milioni moja

Mchezo kwa njia ya mtandao ulio na lengo la kupiga vita njaa, hii leo umeandikisha washiriki wengi zaidi. Mchezo huo ujulikanao kama Freerice.com uliwaandikisha washiriki milioni moja wanaolisha watu walio na njaa duniani kupitia michango yao ya mchele kwa shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

Washirika wa mtanadao huo hadi sasa wamechanga nafaka bilioni 100 tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2007 inayoweza kuwalisha karibu watu milioni tano kwa siku moja. Washiriki wa mtandao huo wanaweza kuchagua maswali 45,000 kwenye masomo tofauti kwa lugha za kiingereza. Kihispania, kitaliano. Kifaransa na kichina. Monica Morara na taarifa kamili.

(SAUTI YA MONICA MORARA)