Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa WFP kuwasaidia wakulima wa mahindi nchini Zimbabwe

Mpango wa WFP kuwasaidia wakulima wa mahindi nchini Zimbabwe

Wakulima nchini Zimbabwe wamerejelea tena kilimo cha mahindi kutokana na mpango unaowasaidia kuuza mazao yao na kupata malipo yao wakati ufaao. Gharama ya juu ya kusafirisha mahindi kwenda kwa mashirika ya nafaka na kushindwa kuwalipa wakulima mapema ni masuala ambayo yamewaweka wakulima kwenye hali ngumu.

Baadhi ya wakulima hawa waliamua kufanya ukulima wa mimiea tofauti kama vile tumbaku hatua ambayo haikuwa nzuri kwao kutoka na ukosefu wa bidhaa zinazohitajika katika kukausha mazao yake. Hata wale wakulima wanaowauzia wanunusi wa kibinafsi bado walalamika kuwa mazao yao hayaleti fedha za kutosha zinazoweza kutosha gharama za kilimo.

George Njogopa na taarifa kamili