Skip to main content

Watoto wazidi kusumbuliwa na utapiamlo nchini Yemen

Watoto wazidi kusumbuliwa na utapiamlo nchini Yemen

Wafanyikazi wa kutoa misaada wanaamini kuwa idadi mpya ya watoto wanaokumbwa na utapiamlo mashariki mwa Yemen huenda ikaeleza hali ilivyo nchini humo na kupelekea wahisani kutoa misaada.

Wizara ya afya nchini Yemen kwa usaidizi wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF walifanyia uchunguzi nyumba 3,104 na kukusanya takwimu kutoka kwa watoto 4,668 walio chini ya miaka mitano. Murtaza Karimjee anafafanua.

(SAUTI YA MURTAZA KARIMJEE)