Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka Sudan Kusini kutoa ulinzi wa kutosha kwa wananchi wa Jonglei ambao wanakabiliwa na tisho la kushambuliwa

UM wataka Sudan Kusini kutoa ulinzi wa kutosha kwa wananchi wa Jonglei ambao wanakabiliwa na tisho la kushambuliwa

Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Sudan Kusini kuchukua hatua ya haraka ili kuwalinda wananchi wa jimbo la Jonglei kufuatia njama zinazopangwa na makundi ya vijana wanaopanga kuwashambulia wananchi hao ikiwa sehemu ya magomvi yao ya mara kwa mara.

Duru zinaeleza kuwa makundi ya vijana yakiwa na silaha kutoka eneo la Lou Nuer yanajiandaa kuwavamia wananachi wa eneo hilo. Hatua hiyo imebainika kufuatia doria iliyofanywa na vikosi vya Umoja wa Mataifa katika eneo hilo UNMISS kubaini njama hizo.

Umoja wa Mataifa umeihimiza serikali ya Sudan Kusini kuhakikisha inawalinda wananchi wa eneo hilo na njama zozote mbaya kutoka kwa wahasama wao.

Maeneo hayo yamekuwa yakijihusisha na ugomvi wa mara kwa mara, ugomvi ambao unadaiwa kuwa na historia ya mifugo na rasilimali nyingine.