Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kutoa chanjo ya polia kwa watoto wa Sudan Kusini

UM kutoa chanjo ya polia kwa watoto wa Sudan Kusini

Mamia ya watoto nchini Sudan Kusini wapo katika mpango wa Umoja wa Mataifa wa utoaji chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo polio.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limetangaza kuendesha kampeni ya siku nne kwa ajili ya utoaji chanjo ya ugonjwa huo.

Mpango huo unatazamia kuwafaidia zaidi ya watoto 370,000. Ili kufanikisha program hiyo UNICEF inatazamia kushirikiana na shirika la afya ulimwenguni WHO. Katika mpango huo lengo kubwa linalozingatiwa na kuwahudumia watoto walio chini ya umri wa miamka 5.