Mfuko wa UM wa msaada wa dharura, CERF wakusanya ahadi za msaada kwa 2012

15 Disemba 2011

Wawakilishi wa serikali kutoka kote duniani wanafanya mkutano wa siku mbili mjini New York kujadili mfuko wa Umoja wa Mataifa wa msaada wa dharura CERF.

Mfuko huo ulianzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2005 ili kuhakikisha kwamba kuna msaada wa fedha wa kukabiliana kwa wakati hali za dharura zinazosababishwa na majanga au vita wakati wowote yanapotokea.

Steve O’Malley mkuu wa sekretariati ya CERF anasema mfuko huo utatoa taarifa kamili ya jinsi ilivyofanya katika miaka yake mitano ya kwanza ya operesheni zake na pia utakusanya ahadi za michango kwa ajili ya mwaka ujao.

(SAUTI YA STEVE O’MALLEY)

Tangu ulipoanzishwa mfuko wa CERF umetoa zaidi ya dola bilioni 2 kwa mashirika ya misaada ya kibinadamu yanayotumika kwenye nchi na mataifa 82 duniani.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter