Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya watoto yasalia kuwa mbaya nchini Yemen: UNICEF

Hali ya watoto yasalia kuwa mbaya nchini Yemen: UNICEF

yali ya watoto nchini YemenShirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limeutaja mwaka 2011 kama mwaka wa kutisha kwa watoto nchini Yemen likiongeza kuwa huenda mwaka 2012 usiwe tofauti ikiwa Yemen haitashughulikiwa kwa njia inayofaa.

UNICEF inasema kuwa itahitaji dola milioni 5o ili kutoa huduma za kibinadamu nchini Yemen na kuongeza oparesheni zake za kusaidia watoto waliothiriwa zaidi na ghasia kwa muda wa miezi 10 iliyopita.

Msemaji wa UNICEF Helen Kadi anasema kuwa kwa sasa UNICEF inasimamia vituo 600 vya matibabu vya kusaidia watoto 44,000 waliokumbwa na utapiamlo. Ameongeza kuwa oparesheni kama hizo zinahitajika kuchukuliwa kama moja ya njia ya keleta utulivu nchini Yemen siku ya za baadaye.