Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima kuwe na mipango kudhibiti kuhama kwa wataalamu wa afya:IOM

Lazima kuwe na mipango kudhibiti kuhama kwa wataalamu wa afya:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji linasema kuna haja ya kuwa na mipango bora ya kudhibiti hali ya wataalamu wa afya kuhama kwenda kufanya kazi nje ya nchi.

Katika warsha maalumu iliyofanyika Ubelgiji IOM inasema hali hii isipopatiwa ufumbuzi basi kuna hatihati ya malengo ya milenia ya afya kutozimizwa hasa katika nchi nyingi zinazoendelea ambako wataalamu hawa wakiwemo wauguzi na madfaktari wanatoka.

Kwa mujibu wa shirika hilo ni maeneo ya vijijini mwa nchi hizo zinazoendelea japo imebainika kwa hata nchi tajiri zimeaanza kuathirika kwa wataalamu wa afya kuhama.

Afisa habari na mawasiliano wa IOM Jumbe Omari Jumbe anafafanua.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)