Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni wakati wa kupambana na saratani ya ufisadi:Ban

Ni wakati wa kupambana na saratani ya ufisadi:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemtaka kila mtu kutimiza wajibu wake ili ktokomeza ufisadi ambao umetawala katika nchi zote na kuwa kikwazo kwa maendeleo ya kijamii na kusababisha ktokuwepo sawa na haki.

Ban akizungumza katika ujumbe maalumu wa siku ya kimataigfa ya kupinga ufisadi ambayo huadhimishwa kila mwaka Desemba 9 amesema, kila mmoja ana jukumu la kuchukua hatua dhidi ya saratani ya ufisadi.

Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na halifu UNODC hakuuna nchi , mkoa au jamii ambayo ina kinga dhidi ya rushwa tatizo ambalo ni uhalifu mkubwa unaorudisha nyuma maendeleo katika jamii zote.

Mwaka huu UNODC na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP wameanzisha kampeni ya pamoja ya kimataifa, inayojikita kuangalia jinsi gani ufisadi unavyokuwa kikwazo cha juhudi za kufikia malengo ya maendeleo ya milenia, unavyoathiri elimu, afya, haki, demokrasia, matarajio na maendeleo.