Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei za chakula zimepungua kidogo:FAO

Bei za chakula zimepungua kidogo:FAO

Mtazamo wa bei ya vyakula uliotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO unaonyesha kuwa mwezi wa Novemba bei hazijabadilika ilikinganishwa na mwezi wa Oktoba.

Katika alama mpya 215 za sasa bei zimepungua kwa asilimia 10 ikilinganishwa na mwezi Februari mwaka huu, ingawa bado ni asilimia moja zaidi ya ilivyokuwa Novemba mwaka 2010. Bei ya nafaka inaonekana kpungua kwa asilimia moja ikilinganisha na mwezi Oktoba na kupungua huko kumetokana na kushuka kwa bei ya ngano. George Njogopa na taarifa kamili.

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)