Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa UM nchini Somalia wawaonya watakaohujumu mpango wa amani

Ujumbe wa UM nchini Somalia wawaonya watakaohujumu mpango wa amani

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia umeonya kuwa yeyote ambaye atajaribu kuhujumu mpango uliokubaliwa kuhusu hatua za kisiasa zinazohitajika ili kuleta amani na udhabiti kwenye nchi hiyo kuwa vitendo vyao havitakubaliwa na jamii ya kimataifa.

Hii ni kwa mujibu wa mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga ambaye amesema kwamba watakaohujumu barabara hiyo ya amani hawatavumiliwa. Mpango huo uliopitishwa kwenye mkutano uliofanyika mjini Mogadishu mwezi Septemba unaeleza hatua zinazostahili kutekelezwa kabla ya kukamilika kwa kipindi cha mpito mwezi Agosti mwaka ujao yakiwemo masuala ya usalama, ya kuundwa katiba mpya na uwiano.