Baraza la haki za binadamu kufanya kikao maalum kuhusu Syria

30 Novemba 2011

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa litafanya kikao maalumu Ijumaa terehe mbili Desemba kutathimini hali ya haki za binadamu nchini Syria baada ya kutolewa ripoti ya tume ya uchunguzi.

Ombi la kikao hicho maalumu limetolewa Jumatano asubuhi na muungano wa Ulaya na kutiwa saini na nchi 28 wanachama wa baraza hilo na nchi 40 ambao ni mataifa watazamaji.

Tarehe 23 Agosti baraza la haki za binadamu lilihitimisha kikao chake cha 17 kwa kupitisha azimio linalotaka kupelekwa Syria tume huru ya kimataifa ya uchunguzi ili kwenda kufuatilia madai ya ukiukwaji wa sheria za kimataifa za haki za binadamu unaofanywa na serikali hiyo ya Kiarabu tangu Machi 2011 na tume ilifanya hivyo na kuwasilisha ripoti yake ya uchunguuzi Jumatatu wiki hii.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter