Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2011 wachukua nafasi ya 10 kama mwaka wenye viwango vya juu vya joto

Mwaka 2011 wachukua nafasi ya 10 kama mwaka wenye viwango vya juu vya joto

Mwaka 2011 umetajwa kuchukua nafasi ya kumi kama mwaka uliokuwa wenye joto la juu zaidi. Miaka mingine 13 yenye joto la juu imeshuhudiwa tangu mwaka 1997. Hii ni kulingana na taarifa ya shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO iliyotolewa hii leo kwenye mkutano wa kimataifa wa hali ya hewa mjini Durban Afrika Kusini.

Viwango vya joto duniani mwaka 2011 vilichochewa na msimu wa La Nina ulioanza kati kati ya mwaka 2010 na kumalizika mwezi Mei mwaka 2011. Michel Jarraud ni katibu mkuu kwenye shirika la WMO.

(SAUTI YA MICHEL JARRAUD)

Bwana Jarraud amaesema kwamba jukumu la WMO ni kutoa ufahamu wa kisayansi na kuwasaidia watoa maamuzi.