Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa ICC akaribisha hatua ya kukamatwa kwa mtoto wa Qadhafi

Rais wa ICC akaribisha hatua ya kukamatwa kwa mtoto wa Qadhafi

Rais wa mkataba wa Roma unaounda mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC amekaribisha hatua ya kukamatwa kwa mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar al-Qadhafi ambaye alikuwa akisakwa na mahakama hiyo.

Saif al-Islam Qadhafi ameripotiwa kutiwa mbaroni na vikosi vya balaza la mpito, katika eneo linalojulikana Obari.

Akizungumzia hatua ya kutiwa kwake mbaroni, rais huyo Christian Wenaweser  amesema kuwa mamlaka za Libya sasa zinakaribisha enzi mpya na kwa kuwaleta kwenze mkonod wa haki wavunjifu wa haki za binadamu.

Ameipongeza mamlaka za Libya kwa hatua hiyo ambayo ameilezea kama ni mashirikiano mema kwa mahakama hiyo  ya ICC.