UNESCO yazindua atlasi

10 Novemba 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulia masuala ya elimu, sayansi na utamaduni UNESCO limezundua atlasi mpya ambayo imelenga kuelezea na kuonyesha jinsi maeneo ya utamaduni wa asili yalivyo hatarini.

Atlas hiyo ambayo imezinduliwa leo mjini Paris ikitumia mfumo wa satalite, imekusudia kufichua na kuonyesha maeneo yote duniani ambayo yanakabiliwa na kitisho cha kutoweka kutokana na mwingiliano wa mambo.

Kwa mujibu UNESCO, atlasi hiyo inakusudia kutoa taarifa muhimu ili kuyasaidia maeneo hayo. Katika miaka ya hivi karibuni matumizi ya atlas kubainisha maeneo yanayoandamwa na hali mbaya yamekuwa shabaya muhimu kwa taasisi mbalimbali za kimataifa.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter