Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaitikia wito wa msaada kwa mataifa ya Amerika ya Kati yanayokabiliwa na mafuriko

WFP yaitikia wito wa msaada kwa mataifa ya Amerika ya Kati yanayokabiliwa na mafuriko

Kurudia kuzuka kwa majanga ya asili kunazidi kutishia usalama wa chakula kwenye maeneo ya vijijini na mijini katika mataifa ya Amerika ya Kati ya Guatemala, El Salvador, Hondurus na Nicaragua mataifa ambayo pia yameathirika na bei kubwa za chakula amesema mkurugenzi wa kanda wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Gemmo Lodesani.

WFP hivi sasa inatoa msaada kwa watu takribani 300,000 walioathirika na mafuriko katika nchi hizo, pia inashirikiana na serikali kufanya tathimini ya chakula ili kujua ni watu wangapi hasa wanahitaji msaada wa chakula na kwa muda gani. Jason Nyakundi anaripoti.