UNHCR yasafirisha misaada kwenda nchini Uturuki

28 Oktoba 2011

Ndege nne zilizosheheni misaada kutoka shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR zinatarajiwa kutua kwenye mji wa Erzurun kuanzia hii leo ili kuwapelekea misaada waathiriwa wa tetemeko la ardhi kwenye eneo la mashariki mwa Uturuki. Ndege ya kwanza inatarajiwa kusafirisha tani 37 kutoka ghala la UNHCR mjini Dubai huku ndege zingine tatu zikitarajiwa kutua kwenye mji wa Erzurum Jumamosi ,Jumapili na Jumatatu mtawalia. Kila ndege itakuwa imesheheni takriban hema 500 na mablanketi 10,000. Misaada mingine itasafirishwa kwenda mji wa Van ambapo wengi wa wenyeji wa mji huo ulio na takriban watu 400,000 walipoteza makao baada ya nyumba zao kuporomoka na kuharibiwa kabisa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter