Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kusambaza misaada nchini El Salvador, Guatemala na Nicaragua

IOM kusambaza misaada nchini El Salvador, Guatemala na Nicaragua

Fedha kutoka kwa mfuko wa huduma za dharura wa Umoja wa Mataifa nchini El Salvado zinasaidia shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kuendelea na usimamizi wa vituo 42 vinavyotoa makao ya muda kwa watu 1,895 kuhakikisha kuwa kuna usafi ya mazingira na pia usambazaji wa misaada miongoni mwa waathiriwa.

Kiasi kikubwa cha mvua ambayo imenyesha kwa muda wa siku kumi kati kati mwa mabara ya Amerika imesababisha vifo vya watu 123 , imeharibu mazao na kuwalazimu maelfu ya watu kuhama makwao. Watu 35 wanaripotiwa kuaga dunia nchini El Salvador na wengine 55,000 kuhama kutoka makwao. Jumbe Omari Jumbe kutoka IOM anafafanua.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)