Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lajadili ripoti kuhusu wanawake, amani na usalama

Baraza la Usalama lajadili ripoti kuhusu wanawake, amani na usalama

Masuala ya UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limejadili ripoti kuhusu wanawake, amani na usalama. Ripoti hiyo inahusu mchango kutoka kwa wanachama 38, mashirika manne ya kimaendeo na idara 27 za Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameshauri nchi wanachama kuongeza idadi ya wanawake kwenye nafasi za juu katika masuala ya kutatua mizozo kwenye ngazi za kimataifa na zisizo za kimataifa. UM umeongoza kwa kuongeza idadi ya wanawake kwenye masuala ya kulinda amani na ya kisiasa.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Amesema kuwa hatua zimepigwa hasa kwenye jimbo la Darfur na Sudan Kusini. Ban ameongeza kuwa kikosi cha kulinda amani kwenye jimbo la Darfur UNAMID kilihakikisha kuwa asilimia 30 ya washiriki kwenye mazungumzo ya amani ya Doha walikuwa ni wanawake.