Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Norway kupoteza kutambuliwa kwake kama mtunzi wa haki za watu wa asili

Norway kupoteza kutambuliwa kwake kama mtunzi wa haki za watu wa asili

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya haki za watu wa asili James Anaya ameonya kuwa ikiwa taifa la Norway litafanyia marekebisho sheria na sera zinazowalenga watu wa jamii ya Sami huenda ikapoteza kutambuliwa kwake kama taifa linaloongoza katika kulinda haki za watu wa asili.

Sami ni watu wa asili wanaoishi Kaskazini mwa Norway na pia nchini Sweden, Finland na Urusi. Anaya amesema kuwa Norway itapoteza heshima imekuwa nayo katika kutambua na kulinda haki za watu wa asili ikiwa bunge la nchi litaidhinisha pendekezo la moja ya vyama vikubwa zaidi nchini humo. Mapendekezo yaliyopelekwa bungeni ni pamoja na kufutiliwa mbali kwa makubalino ya shirika la kazi duniani kuhusu watu wa asili na wa makabila kwenye nchi zilizo huru na pia kufutilia mabli bunge la jamii ya Sami kulingana na vile Rupert Colville kutoka ofisi ya haki za binadamu anavyoeleza.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)