Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto zilizo mbele ya G20 zinahitaji mshikamano na hatua za pamoja:Ban

Changamoto zilizo mbele ya G20 zinahitaji mshikamano na hatua za pamoja:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mataifa ya G20 yana fursa na wajibu wa kihistoria wa kutoa sukluhisho na kuongoza katika kukabili changamoto nyingi zinazoikabili dunia hivi sasa.

Katika barua yake kwa G-20 iliyotolewa kwa vyombo vya habari Ban amesema karibu duniani kote matatizo ndio hali ya kila siku na kuoengeza pamoja na hayo dunia haiwezi kumudu kupoteza mwelekeo kwa wale wanaoathirika zaidi. Amesema hayo ni pamoja na masikini, dunia, vijana na wanawake.

Ameongeza kuwa na wale ambao hawachangii matatizo haya ndio wanaolipa gharama kubwa. Ameyatolea wito mataifa ya G-20 kuongeza mshikamano na kujaribu kupata ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili dunia.