Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani vikali mauaji ya walinda amani wa UNAMID Darfur

Baraza la Usalama lalaani vikali mauaji ya walinda amani wa UNAMID Darfur

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali mashambulizi dhidi ya walinda amani wa vikosi vya pamoja vya Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika UNAMID kwenye jimbo la Darfur Sudan. Mashambulizi hayo yaliyofanyika Oktoba 10 yamekatili maisha ya wanajeshi wawili kutoka Rwanda na mshauri mmoja wa polisi kutoka Senegal. Wanajeshi wengine watano wa Rwanda na Mgambia mmoja wamejerhiwa vibaya katika shambulio hilo.

Katika taarifa maalumu wajumbe wa Baraza la Usalama wamerejea wito wao wa kutaka vikosi vya UNAMID kuungwa mkono na kuzitaka pande zote husika katika mgogoro wa Darfur kutoa ushirikiano unaohitajika kwa vikosi hivyo

(SAUTI KHS UNAMID)