Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taifa la Yemeni lakabiliwa na njaa kubwa wakati pia likikumbwa na matatizo ya kibinadamu

Taifa la Yemeni lakabiliwa na njaa kubwa wakati pia likikumbwa na matatizo ya kibinadamu

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP leo limeonya kwamba kuzorota kwa hali ya usalama wa chakula iliyochangiwa na kupanda kwa bei, upungufu wa mafuta na matatizo ya kisiasa kunazifanya familia nyingi kushindwa kulisha watu wake.

Mkurugenzi mkuu wa WFP Bi Josette Sheeran amesema hasa ongezeko la gharama za chakula na machafuko ya kisiasa yamewaacha mamilioni ya watu katika hali mbaya, huku utapia mlo ukighubika maelfu ya wanawake na watoto. Alice Kariuki anaripoti.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)