Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani yatoa msaada wa kuwasaiadia wanaoishi na virusi vya ukimwi Ethiopia

Marekani yatoa msaada wa kuwasaiadia wanaoishi na virusi vya ukimwi Ethiopia

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limekaribisha msaada wa jumla ya dola milioni 56 kutoka kwa shirika la mpango wa dharura la ukimwi la rais wa Marekani PEPFAR msaada ambao utachangia katika kuongeza ufadhili wa programu za kusaidia watu wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini Ethiopia.

Mkurugenzi mkuu wa WFP Josette Sheeran anasema kuwa misaada ya vyakula inawawezesha wanaoishi na virusi vya ukimwi kuwa na matumaini kwenye maisha yao akiongeza kuwa bila chakula kwao matibabu hayafaulu. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)