Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji waliokwama Sebha Libya waanza safari kurejea nyumbani:IOM

Wahamiaji waliokwama Sebha Libya waanza safari kurejea nyumbani:IOM

Zaidi ya wahamiaji wa Kiafrika 1200 ambao walikuwa wamekwama katika mji wa Sebha Kusini mwa Libya wameanza kuhamishwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na kupelekwa Chad.

Wahamiaji hao wameanza kuondoka Sebha kwa msafara wa malori 15 Jumapili Oktoba pili na safari hiyo inatarajiwa kuchukua siku saba hadi kuwasili Chad. Kundi hilo ni sehemu ya wahamiaji wa Kiafrika 3000 ambao walikuwa wanapata hifadhi kwenye kituo cha muda cha IOM mjini Sebha na wahamiaji hao wanatoka katika nchi 10 tofauti za Afrika. Mapigano makubwa kwenye mji huo ndio yalikuwa kikwazo cha watu hao kuhamisha. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)