Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC kuchunguza mauaji yaliyotekelezwa Ivory Coast:Ocampo

ICC kuchunguza mauaji yaliyotekelezwa Ivory Coast:Ocampo

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC leo Jumatatu imempa idhini mwendesha mashitaka mkuu kuanzisha uchunguzi dhidi ya ghasia na mauaji yaliyofanyika Ivory Coast baada ya uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka jana.

Mwendesha mashitaka huyo Luis Moreno Ocampo aliomba kupewa haki mwezi Juni ya kufanya uchunguzi dhidi ya madai kwamba majeshi yaliyokuwa yanamuunga mkono Rais aliyetolewa madarakani Laurent Gbagbo pamoja na yale ya aliyekuwa mpinzani wake Alassane Ouattara walitekeleza uhalifu wa kivita.

Moreno-Ocampo amesema watu takribani 3000 wameuawa na 520 kuwekwa kizuizini wakati wa machafuko hayo.

(SAUTI YA MORENO OCAMPO)