Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima wa vijijini nchini Ghana na Nicaragua kunufaika na mpango wa UM

Wakulima wa vijijini nchini Ghana na Nicaragua kunufaika na mpango wa UM

Raia kadhaa wa Ghana na Nicaragua ambao wanaishi katika hali ngumu vijijini wanatazamia kupigwa jeki ili kuwasukuma mbele kiuchumi kufuatia mpango wa Umoja wa Mataifa wa ukuzaji uchumi unaotazamiwa kutekekezwa kwenye maeneo hayo. Katika mpango huo unaratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa IFAD, wakulima hao wa maeneo ya vijijini wametengewa kiasi cha dola za kimarekani milioni 31.5 ambazo zitatumika kama injini ya kusuma mbele shughuli za uzalishaji mali.

Mpango kama huo wa utoaji mikopo kwa wakulima wadogo wadogo umetajwa kuleta matunda mema wakati ulipoanza kutekelezwa nchini Ghana miaka 16 iliyopita. Makundi ya wanawake na vijana wanaendesha kilimo kwenye maeneo ya vijijini ndiyo wanatazamiwa kulengwa zaidi na mkopo huo.