Kukabiliana na NCD’s lazima mtazamo wa watu ubadilike:Mponda

28 Septemba 2011

Waziri wa afya wa Tanzania mheshimiwa Haji Mponda amesema ili kukabiliana na maradhi yasiyo ya kuambukiza yaani NCD’s lazima mtazamo wa watu kuhusu maisha ubadilike.

Akizungumza na Radio ya Umoja wa mataifa baada ya kukamilika kwa mjadala wa kimataifa kuhusu maradhi hayo hapa New York, bwana Mponda amesema vyakula vinavyoliwa kila siku ni muhimu sana katika kupunguza hatari ya magonjwa ya kisukari, maradhi ya moyo, saratani na matatizo ya kupumua. Pia amesema mazoezi ya mwili yana nafasi kubwa ya kusaidia kukinga watu na magonjwa hayo.

(SAUTI YA HAJI MPONDA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter