Zimbabwe yazindua mipango ya kitaifa kwa ajili ya watoto na familia:UNICEF

Zimbabwe yazindua mipango ya kitaifa kwa ajili ya watoto na familia:UNICEF

Hatua ya pamoja ya kushughulikia matatizo ya mahitaji muhimu ya yatima na watoto wengine wasiojiweza , serikali ya mseto ya Zimbabwe kwa ushirikiano na jumuiya ya kimataifa ya wahisani inayojumuisha serikali za Uholanzi, Sweden, Uingereza, tume ya Ulaya na hirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, wamezindua mpango kabambe kwa ajili ya watoto wanaohitaji msaada Zimbabwe.

Mpango huo wa kitaifa kwa ajili ya yatima na watoto wengine wasiojiweza awamu ya pili, wa 2011-2015, na kutekelezwa kwa msaada kutoka mfuko wa kuwalinda watoto unajumuisha pia mipango ya kuzisaidia familia kukabiliana na hatari na mshituko wa masuala matatu ambayo ni kuwapa fedha familia masikini, msaada wa kielimu kupitia mpango wa elimu ya msingi na kutoa huduma ya kuwalinda watoto ambao ni waathirika wa kunyanyaswa, ghasia na kunyonywa.