Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa Syrian wametekeleza uhalifu dhidi ya ubinadamu:Botswana (GA-66)

Viongozi wa Syrian wametekeleza uhalifu dhidi ya ubinadamu:Botswana (GA-66)

Viongozi wa Syria wanapaswa kufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kukabiliana na makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waliokuwa wakiandamana kwa amani.

Hivyo ndivyo alivyosema makamu wa Rais wa Botswana Mompati Merafhe alipohutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo Jumatatu. Pia amelikosoa Baraza la Usalama kwa kile alichosema linachelewa na kusitasita kuchukua hatua dhidi ya hali ya Syria.

Amesema tamko la Baraza la Usalama kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu na manyanyaso yanayofanywa na jeshi la nchi hiyo dhidi ya raia limechelewa sana na limeshindwa kuitaka serikali ya Syria kuheshimu haki za binadamu na sheria za kimataifa. Uhalifu dhidi ya ubinadamu umetendeka na uongozi wa Syria unapaswa kujibu mashitaka kupitia ICC, amesema kiongozi huyo.