Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Nigeria na Ban wajadili afya ya uzazi, uharamia na masuala ya usalama

Rais wa Nigeria na Ban wajadili afya ya uzazi, uharamia na masuala ya usalama

Afya ya uzazi, uharamia na usalama wa Afrika Magharibi yamechukua nafasi ya juu katika ajenda ya mazungumzo kati ya Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon na Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan. Ban amempa moyo rais Jonathan, ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kwa kuendelea kusaidia nchi katika kanda hiyo zinayokabiliwa na changamoto za usalama, kama vile Ivory Coast na Liberia.

Pia walibadilishana mawazo kuhusu vita dhidi ya uharamia kwenye Ghuba ya Guinea pamoja na jitihada za kimataifa za kuboresha hali ya afya ya uzazi. Katibu Mkuu pia ametoa shukrani zake kwa msaada wa rias Jonathan na Serikali yake kutokana na mashambulizi ya bomu mwezi uliopita kwenye jengo la Umoja wa Mataifa mjini Abuja ambapo watu 23 waliuawa, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi 11 wa Umoja wa Mataifa.