Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaitaka Sudan kuruhusu misaada kwenye eneo la Kordofan Kusini

WFP yaitaka Sudan kuruhusu misaada kwenye eneo la Kordofan Kusini

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limetoa wito kwa mara nyingine kwa serikali ya Sudan wa kutaka kuruhusiwa kwa wafanyikazi wa kutoa huduma za kibinadamu kuingia eneo la Kordofan Kusini ili kutoa misaada kwa waliohama makwao. WFP inatoa usaidizi kwa maelfu ya watu ambao wamelazimika kuhama makwao kufuatia mapigano kwenye mkoa wa Blue Nile ambapo imetuma chakula cha kuwalisha karibu watu 54,000. Pia kati ya wanaokimbia mapigano kwenye eneo la Blue Nile wanaripotiwa kuvuka mpaka na kuingia nchini Ethiopia.