Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Badr kutembelea kambi za wakimbizi nchini Kenya na Ethiopia

Badr kutembelea kambi za wakimbizi nchini Kenya na Ethiopia

Mkuu wa kamati kuu ya shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Balozi Hisham Badr atatembelea kambi za wakimbizi nchini Ethiopia na Kenya kuanzia juma lijalo kujionea mwenyewe hali ilivyo wakati eneo la pembe linapokumbwa na ukame.

Ziara hiyo inajiri baada ya ziara iliyofanywa na mkuu wa UNHCR Antonio Guterres kwenye pembe ya Afrika mwezi Agosti na pia kabla ya mkutano wa kila mwaka wa UNHCR utakaondaliwa mwezi Oktoba. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)